Dear arrogant politicians
Today I write to you, I know you will read this message. However, I am sure you will ignore or even come in storm against me. It’s time you realized that I am tired! Being a media personality, I will not give you my MIC when you attend to political rallies, Sitawaruhusu mtemee mate MIC zetu za studio...
I will not allow my newsroom Professional Camera to cover your Insightful and dirty images. You mouths are filled with TRIBAL, INSIGHTFUL, & HATE messages. Gatundu South MP Moses Kuria, Nairobi ODM Chairperson George Aladwa, Machakos Senator Johnstone Muthama Nairobi Senator Mike Sonko. Kiambu Governor Hon. William Kabogo Gitau Political analyst Mutahi Ngunyi - Wiseman (unwiseman),This are just but a few who I can mention.
Sijui nani aliwalaani, mpaka maombi mnaharibu!! Matamshi yenu hayana ladha kabisa! Ninachobaki nikijiuliza ni iwapo tunayo idara ya mahakama au la.?? Sijui kama tunaye Jaji Mkuu Dr Willy Mutunga, sijui kama tunayo tume ya uwiano na utangamano NIC inayoongozwa na Francis Ole Kaparo, hata huenda Tume ya Maadili na kupambana na ufisadi EACC yake Keriako Tobiko ilishakufa!
Nikiwa mwanahabari, binafsi sitahudhuria wala kupeperusha taarifa za hawa wanaume niliowataja hapa na wengine ambao hawajatajwa hapa... wala sitakubali stesheni ninayo ihudumia kuhudhuria makongamano ya wanyama hawa.! Naviomba sana vyombo vya habari vyote nchini kuusoma ujumbe wangu.. Citizen TV Kenya Radio Citizen FM NTV Kenya Nation Media Group Royal Media Services The Standard Media Group Radio Africa Limited(Lions Place), Bbc.com/news CNN International Radio Maisha QFM na stesheni zote..
Dawa ya kusaidia jamii ni kukosa kuwapa nafasi watu hawa katika hafla zao. Iwapo vyombo vya habari vitakoma kuwapa nafasi hewani majamaa hawa, basi matamshi yao yatasalia kimya kwa vinywa vyao. Wanauchafua ulimwengu.
Siwezi kutamatisha kauli yangu bila kumkashifu mgombea urais Mtarajiwa nchini Marekani anayetafuta tiketi ya chama cha Republican Donald J. Trump, huyu ni mwanadamu ambaye anastahili kunyimwa tiketi ya Republican iwapo kweli uongozi wa chama cha Republican unaheshimu hadhi ya taifa hilo maarufu ulimwenguni. Jamaa huyu endapo kwa bahati ya ibilisi atapewa tiketi na kwa bahati ya Punda Mchafu akashinda kura, basi ulimwengu mzima utaangamia mikononi mwake.
No comments:
Post a Comment